Mastodon
Local News

Sidney Mamba Afariki dunia

Yasemekana Sidney Mamba mvulana wa miaka 7 aliyegongwa na gari la msafara wa naibu rais William Ruto huko Busia jana, amefariki hospitalini

Naibu rais alisema ofisi yake ilikuwa inashughulika baada ya kumkimbiza hospitalini kuhakikisha maisha ya mvulana huyo yanaokolewa, lakini kwa bahati mbaya aliaga dunia kufuatia majeraha mabaya aliyoyapata.

Wakati akikabidhi kipande cha ekari tano kwa Taasisi ya Maji na Samaki kilichotolewa na Kaunti ya Busia kwa Sisenye, Budalangi, Ruto alisema alisikitishwa mno na kifo chake. “Kufuatia ajali hiyo ya kusikitisha, Sidney amepelekwa kwa matibabu na ofisi yangu inafuatilia kuhakikisha anapata nafuu. Tunamwombea nafuu ya haraka,” alisema naibu rais kupitia Twitter, Ijumaa, Juni 7. Lakini kwa bahati mbaya, Jumamosi, Naibu Rais aliandika na kusema mvulana huyo ameaga dunia na kutuma risala zake za rambirambi kwa familia.

“Nasikitishwa na kifo cha Sidney Mamba Felix, mvulana mdogo mchangamfu. Nilifuatilia kwa karibu hali yake baada ya kufahamishwa kuhusu ajali hiyo, sasa, naomboleza na familia ya Mzee Mamba, rafiki zake kwa kifo chake,” alisema Ruto Jumamosi Juni 8. Mvulana huyo aligongwa na gari katika msafara wa Naibu Rais wakati ukiondoka Kaunti ya Busia baada ya kuzindua mradi wa mabilioni ya pesa wa unyunyiziaji maji huko Budalangi.

Advertisement

Ruto aliandamana na na wanasiasa kadhaa wa eneo hilo kuzindua mradi wa KSh 5.8 bilioni wa ekari 10,000. Mradi huo unatazamiwa kuzifaidi zaidi ya familia 12,000 zinazoishi Port Victoria, Busia.

Tambua Africa Reporter

Blogger and news writer at Tambua Africa News.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Kindly Allow Ads view this page.