Home Local News Watu 3 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Tawa- Mbumbuni kaunti ya...

Watu 3 wafariki katika ajali kwenye barabara ya Tawa- Mbumbuni kaunti ya Makueni

820
0

Watu watatu wamefariki papo hapo huku wengine wawili wakilazwa katika hospitali kufuatia ajali ya barabarani katika barabara ya Tawa- Mbumbuni eneo la Katithi Mbooni Mashariki Makueni asubuhi hii. Akithibitisha hayo kamanda wa polisi kaunti ya Makueni Joseph Ole Napeiyan amesema ajali hiyo imehusisha pikipiki mbili ambazo zimegongana ana kwa ana. Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Tawa majeruhi wakilazwa katika hospitali iyo hiyo. Polisi wanaendesha uchunguzi zaidi.

Previous articleHow much does it cost to advertise on Facebook, Twitter, Linkedin and Youtube?
Next articleClimbing Mt Kenya on a wheelchair
Blogger and news writer at Tambua Africa News.