Akizungumza wakati wa kupokea kilo 35 za dhahabu iliyokuwa imeibwa kutoka nchini humo, Rais wa Tanzania John Magufuli amedokeza kwamba mkataba wa kuizuia Kenya mahindi ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa wakati wa ziara ya Rais Kenyatta nyumbani wake hivi karibuni.
Wakati wa kupokea mzigo huo, Rais Magufuli alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Kenyatta kupitia simu.
Waziri wa Masuala ya Kigeni Monicah Juma, Mkuu wa Mashtaka Noordin Hajj, Mkuu wa Upelelezi George Kinoti na Katibu wa Kilimo Hamadi Mboga ni miongoni mwa waliousindikiza mzigo huo uliobebwa na ndege ya kijeshi. Baadhi ya maafisa hao wanatarajiwa kuendeleza mazungumzo kuhusu mkataba huo wa mahindi na masuala mengine.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kilimo, Hamadi Mboga licha ya wakulima wa eneo la Bonde la Ufa kulalamikia hatua ya kuagizwa mahindi kutoka nje ya nchi, kuna upungufu mkiubwa wa bidhaa hiyo kutokana na kuchelewa kwa msimu wa mvua mwaka huu.
Kwa mujibu wake, Kenya inahitaji mahindi katika magunia zaidi ya milioni 4.3 kila mwezi. Kuanzia mwezi uliopita, baadhi ya wasagaji mahindi wamelazimika kusiyisha shughuli zao kwa kukosa mahindi.
Ikumbukwe, wakulima wa mahindi katika Bonde la Ufa wamekuwa wakipinga mpango wa kununua mahindi katika magunia zaidi ya milioni 12.5 huku wakisistiza  kwamba serikali iweke wazi kiwango cha upungufu na kuhakikisha mahindi yananunuliwa kwanza kabla ya shughuli hiyo kuelekezwa nje ya nchi.
READ
- Sultana 7th February 2023 Full Episode part 1 and 2 Written Updates
- Kenyan Prince reconciles with his girlfriend Princess Kerubo after short break-up
- Grisly Lodwar-Kakuma Highway Accident claim 14 Lives, 12 badly injured
- Babu Owino, We are Not Kids, Uhuru Should Resign as a Peace Envoy and Join Azimio Demos
- Wake up Call by Grauchi #101 – 2023 Afrobeats, Kenyan, Bongo and Dancehall