Advertisement
Local News

KASISI MMOJA NA POLISI

Siku moja kasisi Onesmas alizuru kambi ya chifu na kuona mbaya. nia yake ilikwa ya kuwapongeza askari wa chifu kwa kazi nzuri ya kuweka usalama kijijini kona mbaya.

“Hujambo afande,” Kasisi Onesmus alimwamukua mkubwa wa askari katika kambi hiyo.

“Sijambo Kasisis Onesmas,” askari huyo alijibu huku akishangaa kumwona kasisi kambini mwa chifu. Alidhani kuwa alikuwa ameleta mashtaka lakini alikosea.

“Nimeonelea nije niwasalimie leo, niwapongeze kwa kazi nzuri na kisha niwanunulie chakula cha mchana kama isharanya ya shukrani zangu.”

Advertisement

Mkubwa wa askari pamoja na askari wenzake walishangaa sana. walikuwa hawajawahi pokea pongezo kutoka kwa mtu yeyote. Walikuwa wamezoea kulaumiwa na kukashifiwa.

Waliondoka, mkubwa wa askari na wenzake watatu waliokuwa chni yake. Walielekea karibu na mkahawa uliokuwa kama hatua ishirini kutoka kambini. Kabla hawajaingia kwenye mkahawa kula chakula, Kasisi aliwaambia kuwa kwanza angependa kwenda kuwaonyesha nyumba ya mhalifu hatari kijijini humo. Askari hao walitayarisha bunduki zao tayari kwa mapambano.

Kasisi aliwapeleka hadi katika nyumba ya akina matata. Matata alikuwa kijana wa mtaa hali mashuhuri chokoraa. Kijana huyu alikuwa akiwasumbua sana wakaazi wa kona mbaya kwa uhalifu mdogo mdogo kama vile unyakuzi wa simu na wizi wa vibeti vya akina mama. Mara nyingi askari wa chifu walimkamata na kumwachilia baada ya kumchapa viboko na kumwonya tu, kwani alionekana kama chakaramu. Mara hii alikuwa korokoroni tena na chifu alikuwa ameamua kumpeleka kituo cha polisi ili apelekwe mahakamani.

Walipoingia nyumbani mwa akina matata walimpata mama yake akiwa taabani. Alikuwa amekonda kwa sababu ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ukimwi. Askari hao walimsikitikia sana.

Walitaka kujua jinsi alivyojisaidia kwa upande wa chakula na kodi. Mama huyo waliwaeleza kuwa mume wake ameiaga dunia na kuwa walisaidiwa na mchungaji Onesmas na mtoto wake wa pekee Matata.

“Matata?” Askari hao waliuliza kwa mshangao. “Naam, huyo Matata ambaye mmemshika na sasa mnataka kumpeleka mahakamani akafungwe. Baba yake alifariki akiwa kidato cha tatu, ikabidi aache shule ili aweze kunitunza,” Mama akaeleza

Askari hao walishikwa na masikitiko na huruma nyingi. Mkubwa wa askari hao aliamuru kila mmoja achange shilingi mia tano ili mama yake Matata apate chakula. Vilevile aliamuru Matata akaachiliwe na kuahidi kuwa atamrudisha shule aendelee na masomo. Kwa ushirikiano na mbunge wa eneo hilo waliamua kumweka kwenye mpango wa karo ujulikanao kama C.D.F. Kweli tukijitolea na kuwajibika tunaweza kuleta suluhu kwa matatizo mengi ya kijamii.

IKIWA UNA HADITHI, TAARIFA, AU JAMBO LOLOTE UNGEPENDA KULICHAPISHA KATIKA MTANDAO HUU,,, UKO HURU BORA USIKAIDI SHERIA ZETU. TUMA KWA WHATSAPP 0713606650

SOMA PIA

Tambua Africa Reporter

Blogger and news writer at Tambua Africa News.

Related Articles

Hi! Post Your Comment Here.

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Kindly Allow Ads to view this page.